MGOMO WA MARUBANI WAANZA UJERUMANI

Marubani waanza mgomo nchini UJERUMANI



Marubani wa shirika kubwa la ndege la nchini UJERUMANI, , LUFTHANSA wameanza mgomo mwingine wa siku 2 na kusababisha zaidi ya safari1000 za ndege kusikitishwa kati ya leo na kesho.
Wafanyakazi hao wamekuwa na mfululizo wa migomo wakipinga sheria mpya ya mafao kwa wastaafu wanayodai kwamba inadidimiza maisha ya wastaafu nchini humo.

Viongozi wa shirika hilo wameielezea hatua ya wafanyakazi hao kwa mgomo huo kuwa ni kubwa sana na kutoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo.