MOURINHO; CHELSEA KIKOSI BORA..........SABABU HIZI HAPA.....

Meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinhoamekisifia kikosi chake kwa kusema ndio kikosi bora kwa sasa kutokana na mwenendo mzurialionao na anaamini suala hilo litaendelea kuwapamorari wachezaji wake kucheza kwa kujituma nakuuona kila mchezo kama fainali.

Amesema mpaka sasa kikosi chake kinaongozamsimamo wa ligi ya nchini England, pia kipokatika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wakundi la saba la michuano ya ligi ya mabingwabarani Ulaya, na kingine anachojivunia ni kuwakatika hatua ya robo fainali ya michuano yaCapital One Cup na kucheza kwa kipindi chamiezi minne bila kufungwa hatua ambayoanaichukua kama sehemu kubwa ya mfanikioaliyokua amejiwekea tangu mwanzoni mwamsimu huu.

Lakini meneja huyo kutoka nchini Ureno mesisitiza kuwa tayari kupokea matokeo yoyote ambayo yatapatikama tofauti na mafanikio aliyoyapata kwa kipindi hiki cha miezi minne tangu msimu wa soka wa barani Ulaya ulipoanza mwezi August mwaka huu.