Katika
siku za hivi karibuni picha za mtu ambaye alizikwa ndani ya gari aina
ya Hummer SUV Jeep nchini Nigeria zimekuwa zikienea katika mitandao ya
kijamii na kuzua mjadala miongoni mwa raia wengi wa taifa hilo.
Picha
hizo zilitoka katika mtandao wa twitter wa msichana mmoja raia waKenya anayetumia jina @Sankorie katika mtandao wake ambaye alishangazwa na kusema kuwa wanaume wa Nigeria ni matajiri hadi wengine huzikwa ndani ya magari yenye thamani ya juu,swala ambalo haliwezi kufanyika nchini Kenya.
Je, unadhani ni kweli kwamba mtu anaweza kuzikwa ndani ya gari lake?