![]() |
Rais Robert Mugabe awalaumu baadhi ya wapinzani wake ndani ya chama cha ZANU PF kwa kupanga kumuondoa mamlakani. |
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
amelaumu baadhi ya watu ndani ya chama chake tawala cha ZANU-PF kwamba
wanapanga kumng'oa madarakani.
Mugabe ameahidi kupambana na rushwa ndani ya chama na kukabiliana na maafisa wa chama hicho ambao kazi yao ni kutoa hongo na kupokea rushwa.
Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa.
Kadhalika Mugabe amesema Mujuru ni mwizi anayepanga kumuondoa mamlakani kwa kushirikiana na maafisa wengine wa chama.
Hata hivyo amekanusha madai ya kwamba anataka kujiuzuru na kusema kuwa huo ni upuuzi.
Hivi karibuni afisa mwingine mkuu wa chama tawala, Robert Gumbo aliiambia BBC kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 90 amegeuza chama tawala na kukifanya kama mali yake binafsi.
Bi Mujuru ambaye amekanusha madai hayo alionekana kama mtu ambaye anechukua usukani wa chama kutoka kwa Mugabe ambaye walipigania naye uhuru wa nchi hiyo kutoka mikononi mwa watwala wazungu.