
VINARA Chelsea ambao wanaongoza Ligi Kuu England wakiwa Pointi 6 mbele ya Mabingwa Manchester City Jumamosi ndio watafungua pazia la Mechi za Ligi za Wikiendi wakwa ugenini huko Saint James Park kucheza na Newcastle.
Chelsea, ambao Msimu huu hawajapoteza Mechi ya Ligi, wameshinda Mechi 11 na Sare 3 na Jumatano Usiku waliichapa Tottenham Bao 3-0 bila ya Straika wao hatari Diego Costa ambae alikuwa Kifungoni lakini kwenye Mechi hii atarudi dimbani.
Lakini Meneja wa Newcastle, Alan Pardew, anaamini Chelsea watafungika tu ingawa amekiri ni Timu nzuri.
Newcastle wao wapo Nafasi ya 9 wakiwa Pointi 16 nyuma ya Chelsea.
Baada ya Mechi hii zitafuata Mechi 5 zitakazoanza Saa 12 Jioni na miongoni mwao ni ile ya Stoke City na Arsenal huko Britannia Stadium ambako Arsenal hawajashinda tangu Februari 2010.
Jumatano Arsenal, ambao wako Nafasi ya 6, waliishinda Southampton Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 89 la Alexis Sanchez.
Mechi nyingine ya Saa 12 Jioni ni huko Anfield ambako Liverpool watacheza na Sunderland.
Mechi za Jumamosi zitahitimishwa kwa ile ya Uwanjani Etihad wakati Mabingwa Watetezi Man City watakapoikaribisha Everton ambao wako Nafasi ya 11