NAHODHA wa zamani wa
Manchester United Roy Keane amesema atamaliza bifu lake na aliekuwa
Meneja wa Klabu hiyo Sir Alex Ferguson na kunywa nae chai ikiwa tu
atamuomba samahani kwa kumsema vibaya. Keane, ambae aliondoka Old Trafford Mwaka 2005 baada ya mgongano,
ametoboa msimamo wake huo alipokuwa akihojiwa na Jarida la FourFourTwo.
Alipoulizwa kama yuko tayari kupata Bia na Ferguson, Keane alijibu: “Itakuwa ni Chai. Akiniomba radhi, ndio nitakunywa nae Chai” “Ikiwa Ferguson ataomba radhi, nitafurahi kusahau na kusonga mbele. Kwa kunisema vibaya, nadhani anapaswa kuniomba msamaha.”
Keane aliongeza: “Nilijua siwezi kuondoka vizuri kwa Shampeni na
Maua. Niliona jinsi Bryan Robson na Steve Bruce walivyoondoka, wote
walikuwa Makepteni wazuri lakini sikupendi walivyoondoka.”
Alipoulizwa ikiwa haoni kwamba Mashabiki watamtenga kwa kuchafua Jina
la Ferguson, Keane alijibu: “Ikiwa Mashabiki wa Man United wataona
nilitumikia vizuri, hiyo safi lakini wakihoji hili na Ferguson,
nitawalaani!”