
Siku ya Ukimwi Duniani inaadhimishwa kila tarehe 1 Desemba kama siku maalumu ya kupanua ufahamu kuhusu maafa yanayoletwa na ugonjwa wa Ukimwi.
Desemba mosi
ilichaguliwa kuwa siku ya Ukimwi kutokana na tarehe
hiyo kuwa ndiyo siku ambayo kirusi
cha Ukimwi kilitambulika rasmi mwaka 1981.
Toka mwaka 1981 hadi 2007
watu zaidi ya milioni 25 wameshafariki kutokana na Ukimwi. Mwaka 2007 peke yake
walifariki milioni 2, kati yao watoto 270,000.
Siku hiyo ilichaguliwa
rasmi mwaka 1988 wakati wa Mkutano wa
Dunia wa Mawaziri wa Afya Kuhusu Mpango wa Kuzuia Ukimwi. Kuanzia
hapo siku hiyo imekuwa ikikumbukwa rasmi na serikali, mashirika
yasiyo ya kiserikali, na wanaharakati.
Toka mwaka 1988 hadi 2004, Siku ya Ukimwi
Duniani ilikuwa ikiratibiwa na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Masuala ya Ukimwi (UNAIDS). Mwaka 2005 UNAIDS
ililipa shirika lisilo la kiserikali la Kampeni ya
Ukimwi Duniani (the World AIDS Campaign) wajibu wa kuratibu siku
hiyo.
Kila mwaka siku hiyo hufanyika kwa ujumbe
maalumu. Ujumbe wa mwaka 2005
hadi mwaka 2010 ulikuwa, "Zuia
Ukimwi: Timiza Ahadi".
MAKALA NA;KIJUKUU BLOG