VAN GAAL ASHAMBULIA MAGAZETI KUHUSU KUNUNUA WACHEZAJI!


LOUIS VAN GAAL ameshambulia Magazeti ya Uingereza kwa kuandika kuwa amepewa kitita cha Pauni Milioni 100 kununua Wachezaji wapya ili kuimarisha Kikosi chake.

Van Gaal amewaambia Waandishi kuwa stori za aina hiyo zitaathiri wao wakitaka kununua Wachezaji.

Akiongea na Wanahabari kwenye Mahojiano maalum kwa jili ya Mechi ijayo ya Ligi na Southampton, Van Gaal alitamka: “Nadhani inachefua kuandika namba. Sidhani Ed Woodward [Makamu Mwenyekiti Mtendaji] amesema kuhusu hilo na mimi sijasema.”

Aliongeza: “Ni kuvunja heshima kwa Wachezaji wangu na sitaki kuongea hilo. Nawaamini Wachezaji wangu na tutafanya kazi pamoja!”

Van Gaal pia aliwapasha Waandishi hao kwa kuwaambia Man United haina tatizo la pesa bali wakiingia Sokoni ndio dau huzidi.

Alinena: “Unadhani Southampton inalipa Fedha nyingi kwa Wachezaji wake? Sidhani kwa sababu ni Southampton. Kuna uhusiano Real Madrid na Man United na si Aston Villa na Southampton. ”

Wanahabari hao pia walikumbusha bifu lake na Ronald Koeman Meneja wa sasa wa Southampton ambayo watakutana nayo Mechi ijayo ya Ligi Jumatatu Usiku lakini Van Gaal alitamka Mechi hiyo si yake na Koeman bali ni United na Southampton.

RATIBA:

**Saa za Bongo




Jumamosi Desemba 6

1545 Newcastle v Chelsea

1800 Hull v West Brom

1800 Liverpool v Sunderland

1800 QPR v Burnley

1800 Stoke v Arsenal

1800 Tottenham v Crystal Palace

2030 Man City v Everton

Jumapili Desemba 7

1630 West Ham v Swansea

1900 Aston Villa v Leicester

Jumatatu Desemba 8

2300 Southampton v Man United