BILL GATES ANJWA MAJI YALIYOTOKANA NA KINYESI CHA BINADAMU............tazama video...

Mmiliki wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates anywa maji yaliyotokana na kinyesi cha binaadam kuonyesha teknolojia itakayosaidia maji safi katika nchi zinazoendelea. 
Bill Gates amesema maji "yana ladha nzuri tu kama yale ya chupa niliyowahi kunywa"

Teknolojia hiyo imeungwa mkono na shirika la WaterAid ambalo limesema kuwa itasaidia sana katika maeneo ya miji.Kulingana na shirika hilo la hisani takriban watu millioni 748 hawana maji safi ya kunywa. katika kanda ya video iliyowekwa katika blog yake,Bwana Bill Gates alishuhudia kinyesi cha Binaadamu kikiingizwa katika mtambo huo kabla ya kunywa maji hayo
''Maji hayo ni mazuri sana ikilinganishwa na maji yoyote yale niliokunywa,na baada ya kusomea teknolojia hii nitayanywa kila siku Maji haya ni salama kabisa'',aliandika katika blog yake. Kulingana na mtengenezaji wa mtambo huo Peter Janicki,maji taka hayo huchemshwa kabla ya mvuke wa maji hayo kutengwa na taka ngumu.
 
Taka hizo ngumu baadaye huwekwa katika moto na kutoa mvuke unaoendesha mashine zinazotoa nguvu za umeme kwa mtambo huo na pia kwa wakazi wa eneo hilo.Maji hayo baadaye hutiwa ndani ya mtambo wa kusafisha maji ili kutoa maji safi ya kunywa.