
Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, sasa maarufu kama Capital One Cup, kati ya Tottenham na Sheffield United ilimalizika kwa Tottenham kushinda kwa Bao 1-0 kwa Bao la Penati Uwanja wa White Hart Lane Jana Usiku.
Penati hiyo ilitolewa Dakka ya 75 baada ya Jay McEveley kuushika Mpira na Andros Townsend kupiga Penati hiyo na kufunga.
Timu hizi zitarudiana tena Wiki ijayo Nyumbani kwa Sheffield United.
VIKOSI:
TOTTENHAM: Vorm, Walker, Dier, Vertonghen, Davies; Townsend, Mason, Stambouli, Eriksen; Adebayor, Kane.
Akiba: Friedel, Kaboul, Rose, Dembele, Lennon, Paulinho, Soldado.
SHEFFIELD UNITED: Howard; Harris, Reed, Basham, McEveley; Doyle, Flynn, Campbell-Ryce; Scougall, Murphy, McNulty
Akiba: Alcock, Baxter, Higdon, Turner, Kennedy, Adams, Wallace
REFA: Neil Swarbrick
CAPITAL ONE CUP
RATIBA
++Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu
Jumanne Januari 20
Liverpool 1 Chelsea 1
Jumatano Januari 21
Tottenham 1 Sheffield United 0
Marudiano
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Jumanne Januari 27
Chelsea v Liverpool [1-1]
Jumatano Januari 28
Sheffield United v Tottenham [0-1]
FAINALI
Jumapili 1 Machi 2015
Liverpool au Chelsea v Tottenham au Sheffield United
****FAHAMU:
-Kwenye Nusu Fainali, ikiwa Timu zìtakuwa Sare na pia kufungana kwa Magoli katika Mechi zao 2, utachezwa Muda wa Nyongeza wa Dakika 30.
-Baada ya muda huo, ikiwa Mechi bado ni Sare basi ile Sheria ya Bao la Ugenini kuhesabika Mawili itatumika.
-Endapo hata ikitumika Sheria ya Bao la Ugenini kuwa Mawili bado Timu zinabaki Sare, Mshindi atapatikana kwa Mikwaju ya Penati 5.