
Mechi
hiyo ambayo ilipigwa jijini London katika dimba la Stamford Bridge
imemalizika muda mfupi uliopita huku Chelsea wakiweza kuendelea
kuustawisha uongozi wao kwenye msimamo wa ligi.
Matokeo
ya mechi hiyo ni sare ya 1-1 ambayo imeendelea kuipa Chelsea uongozi wa
pointi 5 zaidi ya Man City wanaoshika nafasi ya pili.
Chelsea walianza kufunga goli kupitia Loic Remy ambaye alimalizia kazi
nzuri ya Eden Hazard katika dakika ya 40 – lakini muda mfupi baadae
David Silva akaisawazishia City baada ya kumalizia pasi ya Sergio
Aguero.
Mpaka mwisho wa mchezo huo matokeo yalikuwa yakisomeka 1-1.

