
STRAIKA wa Chelsea Diego Costa ambae alifunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa Kosa la Mchezo wa Vurugu kufuatia kumkanyaga Beki wa Liverpool Emre Can kwenye Mechi ya Marudiano ya Nusu Fainali ya Capital One Cup dhidi ya Liverpool Jumanne Usiku, ameamua kupinga Mashitaka hayo.
Kwenye Mechi hiyo ambayo Chelsea waliifunga Liverpool 1-0 na kutinga
Fainali, Costa ameshitakiwa kwa kumtimba kwa makusudi Beki wa Liverpool
Emre Can katika Dakika ya 12 ya Mechi hiyo.
Costa anatarajiwa kulikabili Jopo Huru la Watu Watatu la FA Ijumaa
Asubuhi na ikiwa Kamisheni hiyo itamsafisha basi atakuwa ruksa Jumamosi
kuwakabili Mabingwa wa England, Manchester City, Uwanjani Stamford
Bridge kwenye Mechi ya Ligi Kuu England inayozikutanisha Timu za Kwanza
na za Pili huku Chelsea wakiwa mbele kwa Pointi 5
Ikiwa Jopo hilo litampta na hatia, Costa atafungiwa Mechi 3 kuanzia hiyo
na Man City na nyingine ni zile dhidi ya Aston Villa na Everton.
