Kisukari Ni Nini?
Kisukari
ni ugonjwa unaotokana namtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye
damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe
kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati.
Wagonjwa wengi wa kisukari hufa kutokana na mshtuko wa moyo au kiharusi.
UGONJWA wa kisukari unaongezeka haraka sana hivi kwamba umekuwa
janga la ulimwenguni pote. Kuna aina mbili kuu za kisukari. Aina ya kwanza
huanza hasa utotoni, na kufikia sasa madaktari hawajui jinsi ya kuizuia.
Makala hii inazungumzia aina ya pili, ambayo imeathiri asilimia
90 ya watu walio na kisukari. Ingawa zamani aina ya pili ya kisukari
ilihusianishwa tu na watu wazima, hivi karibuni imewaathiri pia watoto. Lakini
wataalamu wanasema kwamba mtu anaweza kujikinga ili asipatwe na kisukari.
Huenda ukafaidika kujua habari Fulani kuhusu ugonjwa huu hatari.
Mafuta mengi kupita kiasi mwilini huchangia sana kisukari.
Wataalamu wanaamini kwamba mafuta yaliyokusanyika tumboni na kiunoni ni ishara
ya uwezekano wa kupatwa na kisukari. Kihususani, mafuta katika kongosho na ini
huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu. Unawezaje
kuepuka kupatwa na kisukari?
Hatua Tatu Zinazoweza Kukusaidia Usipatwe na Kisukari
1. Pimwa kiwango cha sukari kwenye damu ikiwa una uwezekano mkubwa
wa kupata kisukari.
Mara nyingi aina
ya pili ya kisukari huanza baada ya hatua inayoitwa prediabetes, yaani, ongezeko la kiwango cha
sukari kwenye damu.
Hatua hiyo ni hatari kama tu kisukari, lakini kuna tofauti:
Ingawa ugonjwa wa kisukari unaweza kudhibitiwa,
hauwezi kutibiwa. Kwa upande mwingine, watu walio na kiwango cha
juu cha sukari kwenye damu wamefaulu
kukipunguza. Huenda mtu asitambue dalili za ongezeko la sukari
kwenye damu. Kulingana na ripoti mbalimbali,
karibu watu milioni 316 duniani pote wana kiwango kikubwa cha
sukari kwenye damu; ingawa wengi wao hawajui wana kiwango hicho. Kwa mfano,
nchini Marekani pekee asilimia 90 ya watu wenye sukari nyingi kwenye damu
hawatambui kama wana tatizo hilo.
Ingawa hivyo, ongezeko la sukari kwenye damu ni hatari. Mbali na
kuwa kisababishi cha kisukari, hali hiyo imehusianishwa na hatari ya kupatwa na
ugonjwa wa akili uitwao dementia. Kama wewe ni mnene kupita kiasi,
hufanyi mazoezi kwa ukawaida, au una watu wa ukoo walio na
kisukari, huenda tayari una kiwango cha juu cha sukari kwenye damu. Unaweza
kujua kiwango chako cha sukari ukipimwa damu.
2. Kula vyakula vyenye lishe.
Unaweza kufaidika ukifanyamamboyafuatayo: Punguza kiasi cha
chakula unachokula.nBadala ya kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi au vinywaji
vyenye kaboni kama vile soda, kunywa maji, chai, au kahawa. Kula vyakula vya
nafaka ambayo haijakobolewa badala ya vyakula vilivyochujwa sana viwandani.
Kula nyama isiyo na mafuta mengi, samaki, njugu, karanga, na maharagwe.
3. Fanya mazoezi.
Kufanya mazoezi kunaweza kupunguza kiwango cha sukari kwenye
damu na kukusaidia uwe na uzito unaofaa. Mtaalamu fulani anapendekeza kupunguza
muda unaotumia kutazama televisheni ili uwe na muda wa kufanya mazoezi. Huwezi
kubadili chembe zako za urithi, lakini unaweza kubadili maisha yako. Utafaidika
sana ikiwa utajitahidi kutunza afya yako
‘NILICHUKUA HATUA!’
Mahojiano
Ulijuaje
kwamba ulikabili hatari ya kupatwa na kisukari?
Nilipofanyiwa uchunguzi wa kitiba kabla ya kuanza kazi mpya,
daktari aliniambia ningepatwa na kisukari ikiwa nisingechukua hatua. Nilikuwa
na mambo manne yanayochangia kisukari:
Nilitoka kwenye jamii ya watu wanaopatwa sana na kisukari, watu
wangu wa ukoowalikuwa na kisukari, nilikuwa mnene kupita kiasi, na sikufanya
mazoezi. Kwa kuwa singebadili mambo mawili ya kwanza, niliamua kurekebisha
mambo mawili ya mwisho.
Ulifanya
nini?
Nilienda kumwona mtaalamu wa kisukari ambaye alinifafanulia
uhusiano kati ya vyakula, mazoezi, uzito,
na kisukari. Niliamua kubadili maisha yangu. Nikaanza kula mboga
kabla ya kula chakula kingine. Hilo lilinipunguzia njaa hivyo sikula sana. Pia,
nilianza kufanya mazoezi, jambo ambalo nilikuwa nimepuuza kwa miaka mingi.
Je,
ulifaulu?
Kwa kipindi cha miezi 18, nilipunguza asilimia kumi ya uzani
wangu, na ninahisi vizuri sana. Nimeazimia kwamba sitaishi tena kama zamani.
Hupaswi kucheza na kisukariCredit;DR Manyanda