
HALMASHAURI
ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga imedhamiria kuyafikisha Mahakamani Makampuni
11 yanayofanya kazi katika Mgodi wa Acacia Buzwagi kwa kosa la kukaidi
kulipa kodi ya huduma ( Service leav) katika Halmashauri hiyo.
Hayo
yamebainika jana katika kikao cha baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa
Kahama baada ya madiwani kutaka kujua
mapato na matumizi ya Halmashauri kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita ikiwa
ni sambamba na kujua kama makampuni hayo yamelipa kodi hiyo ya huduma .
Akitolea
ufafanuzi suala hilo Mweka hazina wa Halmashauri hiyo Wilfred Kishere amesema
kuwa kuna baadhi ya makampuni yamekuwa yakikaidi kukaguliwa kwa lengo la kuona
faida wanayoipata hali ambayo inaleta ugumu kukadiria aslimia 0.3 ya
faida wanayoipata ili kuweza kuilipa Halmashjauri husika.
Kishere
aliyataja Makampuni hayo kuwa ni pamoja na Mafinga Best, Shimiyu
Constraction, Isamilo Supplies, Gorden Valley Hotel, G4S security Services,
Fresters Investment Company Limited, Beb Company Limited, Agreco Project
, AGB Eqipment pamoja na Kasekdindis Contraction.
Sambamba
na hayo madiwani hao wametoa masikitiko yao kwa watumishi wa Halmashauri ya mji
wa Kahama kuwa pamoja na kuwa na vyanzo vingi vya mapato wamekuwa mazembe
katika kukusanya mapato ya ndani.
Mmoja
wa Madiwani hao Aoko Nyangusu amesema kuwa watumushi wa Halmashuri hiyo
wamekuwa wakikaa ofisini bila ya kukusanya mapato huku akisisitiza kuwa kuna
baadhi ya wafanyabiashara hawana leseni za kufanya shughuli hizo.
Aidha
Diwani huyo alisema kuwa Halmashauri hiyo imekuwa haifikii malengo ya kukusanya
mapato ya ndani kutokana na uzembe unaofanywa na wahasibu hao kwa kutokukusanya
mapato hali ambayo halmashuri imekuwa haina fedha za kutosha hata za kuwalipa
wakandarasi wanaoidai.