MAKOMANDOO 30 WAUAWA NCHINI UFILIPINO



Makomandoo 30 wauwawa nchini PHILIPPINES
 
Makomandoo 30 wa jeshi la Polisi nchini PHILIPPINES wameuawa baada ya kutokea mapigano makali kati ya waasi na jeshi hilo katika jimbo la MIANDANAO, lililoko kusini mwa nchi hiyo.
Mapigano hayo yalizuka baada ya jeshi la PHILIPPINES kufanya shambulio la kushitukiza katika kijiji kimoja kinachodhibitiwa na wapiganaji wa kiislamu wa kikundi cha MAOIST.

Jeshi la PHILIPPINES limepeleka kikosi cha kutuliza ghasia katika kijiji hicho ili kuhakikisha kuwa hakuna maisha ya raia zaidi yanayopotea.