
Mwanamke
mmoja Schorastica Shija (55) mkazi wa Mtaa wa Kitwana kata ya Busoka
wilayani Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kwa kukatwa kwa mapanga kichwani
na watu wasiojulikana kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa Kimapenzi.
Akizungumza
na suala hilo afisa mtendaji wa Mataa huo, Rafael Jumanne alisema tukio hilo
lilitokea juzi majira ya saa tano usiku wakati Scholastica shija
akiwa numbani kwake anajiandaa kulala akiwa na wajukuu zake wawili.
Alisema
baada ya majambazi hayyo ambao idadi yao haikufahamiaka, walianza kumcharanga
mapanga kichwani na mkono wa kulia hali ambayo ilisababisha kuvuja kwa
damu nyingi na baadaye kifariki dunia.
“Nilipigiwa
simu majira ya saa tano usuku na mwenyekiti wangu wa Mtaa na baada ya
kufika eneo la tukio nilikuta tayari ameshaaga dunia
huku damu nyingi zikiwa zinaendelea kuvuja kwa wingi”.alisema Jumanne.
Afisa
Mtendaji huyo alisema chanzo cha mauji hayo bado
haijafahamika ingawa zinahusishwa na wivu wa kimapenzi na
kwamba jeshi la Polisi lilifika eneo la Tukio na kuupeleka mwili wa
maraehemu katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya
Kahama.
Alisema
Mbali na maujai hayo, pia baiskeli moja aliibiwa na majambazi
hayo huku hakuna mtu yeyote ambaye alikamatwa kuhusiana na tukio
hilo na kwamba watashirikiana na jeshinla Polisi kufanya upelelezi.
Akizumgumza
kwa nja ya Simu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shimyanga Justus Kamugisha
alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo na hakuana anayeshikiliwa huku
upelelezi unaendelea kufanyika ili kuwabaini na hatimaye kuwafikisha
katika sheria.
Kamanda
kamugisha aliwataka wananchi kuacha kuamini imani za Kishirikia ambazo
kimsingi zinaleta uchochezi wa mauaji ya vikongwe huku akiitaka
jamii ishirikiane na jeshi la Polisi kuwafichua.