Ishu ya mgogoro wa rapper Lil Wayne na YMCMB sasa umefikia mbali na time
hii jamaa amefungua mashtaka alipwe dola za Marekani milioni 51 na
msanii mwenzake Birdman.
Lil Wayne amemtaka jaji kuvunja mkataba
wa lebel yao kwa kuwa hawajamlipa fedha zake ili awe huru kufanya mambo
yake baada ya kundi hilo kushindwa kufanikisha Wayne kuachia album yake
ya ‘Tha Carter V‘.
Mwanzoni mwa wiki hii Lily Wayne alinukuliwa
akisema baada ya Cash Money kushindwa kumlipa pesa zake, ataondoka ndani
ya kundi pamoja na wasanii Nick Minaj pamoja na Drake.