RONALDO ATWAA FIFA Ballon d'Or 2014, JOACHIM LOEW KOCHA BORA NA GOLI BORA NI LA RODRIGUEZ

RONALDO-BORA-DUNIANI2014
CRISTIANO RONALDO, kwa Mwaka wa Pili mfululizo ameshinda FIFA Ballon d'Or ambayo ni Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2014 na kuwafunika Wapinzake wake Lionel Messi na Manuel Neuer.
 
Ronaldo alitangazwa Mshindi kwenye Hafla iliyofanyika Leo hii huko Ukumbi wa Kongresshaus Jijini Zurich huko Uswisi na hii ni mara ya 3 kwake kuizoa Tuzo hii ambayo Messi anaongoza kwa kuitwaa mara 4.

Kwa upande wa Kinamama, Mchezaji Bora ni Nadine Kessler wa Germany.
 
Tuzo ya Goli Bora la Mwaka imeenda kwa Mchezaji mwenzake Ronaldo wa Klabu ya Real Madrid, James Rodriguez, kwa Goli lake aliloifungia Nchi yake Colombia ilipocheza na Uruguay.

Kocha Bora wa Mwaka ni Joachim Low wa Mabingwa wa Dunia Germany.

Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Kipa Manuel Neuer wote pia walitajwa kwenye Listi ya Wachezaji 11 wa Kikosi Bora cha Mwaka, FIFA/FIFPro World XI, pamoja na Mabeki Phillip Lahm, David Luiz, Thiago Silva and Sergio Ramos, Viungo Andres Iniesta, Toni Kroos na Angel Di Maria pamoja na Fowadi Arjen Robben.

Hafla ya Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani ilianzishwa Mwaka 1991 lakini Mwaka 2010 iliunganishwa na ile ya Jarida la France Football, Ballon d'Or, na 

Tuzo zilizotolewa:
FIFA Ballon d’Or==Cristiano Ronaldo 

FIFA Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Mwanamke==Nadine Kessler


FIFA Kocha Bora wa Mwaka Wanaume==Joachim Low 


FIFA Kocha Bora wa Mwaka Wanawake==
Ralf Kellermann 

FIFA Tuzo ya Rais [Presidential Award]==Hiroshi Kagawa 


FIFA Tuzo ya Uchezaji Haki [Fair Play Award]==
Wanaojitolea FIFA


FIFA Tuzo ya Goli Bora la Mwaka [Puskas Award]==
Jame Rodriguez 


FIFA/FIFPro World XI Kikosi Bora cha Mwaka==

-Kipa: Manuel Neuer (Germany/Bayern Munich), 

-Mabeki: Sergio Ramos (Spain/Real Madrid), David Luiz (Brazil/PSG), Philipp Lahm (Germany/Bayern Munich), Thiago Silva (Brazil/PSG), 

-Viungo: Andres Iniesta (Spain/Barcelona), Toni Kroos (Germany/Real Madrid), Angel Di Maria (Argentina/Manchester United)

-Mafowadi: Arjen Robben (Netherlands/Bayern Munich), Lionel Messi (Argentina/Barcelona), Cristiano Ronaldo (Portugal/Real Madrid). 

WASHINDI WALIOPITA WA Ballon d'Or:
1956 Stanley Matthews
1957 Alfredo Di Stefano
1958 Raymond Kopa
1959 Alfredo Di Stefano
1960 Luis Suarez
1961 Omar Sivori
1962 Josef Masopust
1963 Lev Yashin
1964 Denis Law
1965 Eusebio
1966 Bobby Charlton
1967 Florian Albert
1968 George Best
1969 Gianni Rivera
1970 Gerd Muller
1971 Johan Cruyff
1972 Franz Beckenbauer
1973 Johan Cruyff
1974 Johan Cruyff
1975 Oleg Blokhin
1976 Franz Beckenbauer
1977 Allan Simonsen
1978 Kevin Keegan
1979 Kevin Keegan
1980 Karl-Heinz Rummenigge
1981 Karl-Heinz Rummenigge
1982 Paolo Rossi
1983 Michel Platini
1984 Michel Platini
1985 Michel Platini
1986 Igor Belanov
1987 Ruud Gullit
1988 Marco van Basten
1989 Marco van Basten
1990 Lothar Matthaus
1991 Jean-Pierre Papin
1992 Marco van Basten
1993 Roberto Baggio
1994 Hristo Stoichkov
1995 George Weah
1996 Matthias Sammer
1997 Ronaldo
1998 Zinedine Zidane
1999 Rivldo
2000 Luis Figo
2001 Michael Owen
2002 Ronaldo
2003 Pavel Nedved
2004 Andriy Shevchenko
2005 Ronaldinho
2006 Fabio Cannavaro
2007 Kaka
2008 Cristiano Ronaldo
2009 Lionel Messi
2010 Lionel Messi
2011 Lionel Messi
2012 Lionel Messi
2013 Cristiano Ronaldo