CRISTIANO Ronaldo amewaomba radhi
mashabiki wa Real Madrid kufuatia timu hiyo kuvuliwa ubingwa wa kombe
la Mfalme dhidi ya mahasimu wao wa mji, Atletico Madrid.
Ronaldo aliwaonesha mashabiki
wake tuzo yake ya tatu ya Ballon d’Or kabla ya kuanza kwa mechi ya jana
usiku ya hatua ya 16 uwanja wa Bernabeu ambapo Real walikuwa wanajaribu
kubadili kipigo cha 2-0 walichopata uwanja wa Vicente Calderon.
Ingawa Fernando Torres alifunga
mabao mawili, Sergio Ramos na Ronaldo walisawazisha, lakini Atletico
walifuzu hatua ya robo fainali kwa wastani wa mabao 4-2 na watachauana
na Barcelona.
“Haiwezekani kuwa vizuri kila mechi kwa asilimia 100,” Mshambulizi huyo wa Ureno aliwaambia waandishi wa habari.
“Sitoki sayari nyingine”,
aliongeza nyota huyo mwenye miaka 29. “kwa niaba ya timu naomba radhi,
labda tungeweza kufanya kitu kizuri zaidi”.
“Siku zote kupoteza sio jambo zuri, lakini lazima ukubaliane nalo”.
“Timu itarudi kwenye kiwango chake na tuna nafasi ya kushinda La Liga na ligi ya mabingwa”