
MKUU WA WILAYA YA KAHAMA BENSON MPESYA.
SERIKALI
wilayani Kahama mkoani Shinyanga imepiga marufuku wananchi wa kijiji cha namba
tisa kata ya Bulyanhulu wlayani hapa kutumia maji ya visima pamoja na kuendesha
shughuli za kilimo kufuatia kuvuja kwa bwawa la maji ya mgodi wa Dhahabu wa
ACACIA Bulyanhulu yanayosadikiwa kuwa na sumu ya Syned.
Akizungumza
na wandishi wa Habari mkuu wa wilaya ya Kahama,Benson Mpesya alisema serikali
imeamua kupiga marufuku utumiaji wa visima vya maji pamoja na shughuli za
kilimo katika kijiji hicho mpaka mpaka baraza la Usimamizi wa mazingira(NEMC)
itakapomaliza uchunguzi kuhusu kemikali hizo.
Mpesya
alisema kufuatia bwawa hilo kujaa maji na kutiririka katika kijiji hicho
kilichopo jirani na mgodi huo uongozi wa kampuni ya ACACIA iliamua kufunga
mabomba sita ya maji kutoka katika mgodi huo kwenda kwenye kijiji hicho huku
kwa lengo la kuwasaidia wananchi mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema kuwa bwawa hilo lilianza kutiririsha maji hayo tangu
tarehe 9/01/2015 kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyonyesha yenye milimita 50 na
hivyo kusababisha bwawa hilo kufurika na maji yake kuelekea katika kijiji
jirani cha namba tisa.
Hata
hivo Mpesya alisema kijiji hicho ambacho kipo ndani ya leseni ya mwekezaji wa
kampuni ya hiyo ambapo bado haijalipa wananchi fidia kilikuwa na jumlaya kaya
tatu zenye watu wapatao 27 huku madhara yaliyotokea ni kukauka kwa mazao na
maji kubadirika rangi tofauti na yalivyokuwa hapo awali.
Mpesya
alisema kufuatia hali hiyo kampuni ya ACACIA ilamua kuwapeleka Jumla ya
wananchi 138 katika hospiatli ya wilaya ya Kahama kwa uchunguzi huku matokeo ya
vipimo yakionyesha hakuna aliyeathirika na madawa hayo mbali ya kukutwa na
magonjwa mengine ya kawaida.
Pia
Mpesya alisema ameunda kamati ya kuangalia hasara zilizotokea kwa wananchi na
kama ni mazao au watu zitaonekana mgodi huo utawalipa fidia wananchi hao ili
kuendelea kuwa namahusiano mazuri baina ya mwekezaji na wananchi wanaoishi
jirani na mgodi huo.
Kwa
upande wake Afisa usalama wa mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Abdallah Mssika
akiongea kwa niaba ya msemaji wa mgodi huo alisema kufuatia kutokea kwa
tukio hilo uongozi umeimarisha miundombinu ya visima na kwamba hali hiyo
haiwezikujirudia tena.
Alisema
mabwawa yamekarabatiwa katika kiwango cha hali ya juu na kuongeza kuwa mabomba
hayo sita waliyoyapeleka katika kijiji hicho ni ya kudumu hivyo wananchi
hawatatumia maji ya visima tena kama siku za nyuma huku wakisubiri ripoti ya
NEMC kutoa majibu sahihi juu ya uchunguzi kemikali hizo.
Credit;kijukuu cha bibi k blog