
Hii itakuwa rahisi sana mtu wangu, hivi mara ngapi umeshawahi kwenda sehemu ukakutana na maandishi ambayo umeshindwa kuyaelewa?
Teknolojia
imekuwa msaada kwenye mengi mtu wangu, pata picha unasafiri kwa mara ya
kwanza kwenda China, unaingia mgahawani, unapewa menu imeandikwa
kichina, unaanzia wapi kwanza?
Google wanatusogeza hapa, google translate app itakusaidia
kama unayumia smartphone yako unaweka app hiyo halafu unaanza kuitumia,
mfano unakutana na bango lenye maandishi unafungua app, unaionyesha
camera ya simu kwenye maandishi hayo unapiga picha, kwenye kioo cha simu
inakuonyesha maana ya neno hilo!

Mbali
na hivyo app hiyo inaweza kukutafsiria kwa sauti hata kile ambacho mtu
anakiongea, yenyewe inakupa tafsiri kwa lugha unayotaka.
Ni
rahisi tu, hauhitaji kuwa na internet ili uitumie, ni app ambayo
inafanya kazi hata kama huna bundle mtu wangu, inapatikana bure kwa
wanaotumia android na iPhone pia.
Cheki app hiyo kwenye video hii.