
PICHA HII SI UASILIA WA HALI YA KILIMA.
Zaidi ya wanafunzi 1200
katika shule za msingi Kilima A, na B, Kata ya Nyihogo halimshauri ya mji wa
Kahama mkoani Shinyanga wanakaa chini
kutokana na shule hizo kuwa na uhaba wa madawati kwa muda mrefu licha ya kuwa katikakati ya mji.
Hali hiyo ilibainika wakati
wa ziara ya baadhi ya viongozi wa Kata ya Nyihogo kufika shuleni hapo kujionea hali ya miundombinu iliyopo na
kukuta idadi kubwa ya wanafunzi wakikaa
chini kwa zamu.
Akizugumzia hali hiyo
Mwalimu Mkuu wa Shule Msingi Kilima A,
Francisca Kisaka alisema shule hiyo inajuma ya wanafunzi 1200, Madawati 100
ambapo wanaokalia madawati ni wanafunzi 300 pekee huku wanafunzi 900 wakiwa
wanakaa chinikwenye sakafu.
Alisema kutokana na ukosefu wa madawati, baadhi ya
madarasa yamekuwa hayatumiki na badala yake yanatumika katika kuhifadhi kuni
huku shule hiyo ikikosa pia choo cha walimu hali ambayo inawalazimu kutumia
vyoo vya wanafunzi.
Naye mwalimu mkuu wa shule
ya msingi Kilima B, Restiel Mlay alisema shule hiyo inajumla ya wanafunzi 1165,ambapo wanaokaa chini ni zaidi ya 300, kutokana na
shule hiyo kuwa na ukosefu wa madawati 107.
Alisema shule hiyo pia
inakabiliwa na uharibifu wa milango
mablimbali hasa katika vyoo
kutokana na kuwepo kwa vijana wanaotumia eneo hilo kuvuta bangi na uhalifu mwingine, huku jamii inayozunguka
eneo hilo kutumia vyoo vya shule kujisaidia.
Hata hivyo shule hizo mbili
zinakabiliwa na ukosefu wa nyumba za walimu,
pamoja na Ofisi ya walimu hali ambayo wanatumia ofisi moja na wakuu wa shule hivyo serikali inapaswa kufanya juhudi za makududi
kukalibilana na changamito hizo.
Diwani wa Kata ya ya Nyihogo
Amos Spemba aliitupia lawama kamati ya
shule hizo kwa kushindwa kuweka mpango kazi madhubuti ya kutatua kero hizo na kwamba ameahidi kulifanyia kazi na
hatimaye kwa kulifikisha katika halamshauri husika.
Afisa mtendaji wa mtaa wa
huo Simon Mabumba aliwataka walimu wakuu kukaa
na kamati ya shule na kufanya kikao na wazazi ili kuwashirikisha kuchangia
maendeleo ya shule, jambo ambali liliungwa mkono na Mratibu elimu wa Kata
hiyo Winifrida Madata.
credit;kijukuu cha bibi k blog