WAZIRI PROFESA MUHONGO AJIUZULU KUHUSIANA NA SAKATA LA ESCROW



Breaking News
Bunge la Tanzania linaanza vikao vyake wiki ijayo, moja ya ishu ambayo wanasiasa na wanaharakati mbalimbali wamekuwa wakishinikiza kufanyiwa maamuzi ni ishu ya Escrow, mwezi DECEMBER, 2014 Rais Kikwete alitangaza kumsimamisha kazi Waziri Anna Tibaijuka kutokana na ishu ya fedha za Escrow ambazo kulikuwa na utata kwamba ni za umma ama za IPTL.

Vuguvugu lililobaki likawa kuwawajibisha Prof. Muhongo pamoja na Wenyeviti watatu wa Kamati za Bunge ambao walitajwa pia kuingiziwa pesa hizo, leo Prof. Muhongo ameitisha kikao na waandishi wa Habari ofisini kwake na kutangaza kujiuzulu nafasi ya Uwaziri