Kundi la wanamgambo wa al Shabab limetishia kuvishambulia vituo viwili vikuu vya kibiashara nchini Ufaransa.
Kanali ya televisheni ya M6 info imeripoti kuwa, kundi la wanamgambo wa al Shabab linaloendesha harakati zake Afrika limetoa mkanda wa video na kutishia kuwa, litavishambulai vituo viwili vikubwa vya kibiashara vya nchini Ufaransa.
Vituo viwili vya kibiashara na kile kinachojulikana kwa jina la Le Forum des Halles ambavyo vinahesabiwa kuwa moja ya vituo muhimu vya kiuchumi vya Ufaransa viko katika mji mkuu wa nchi hiyo Paris.
Ufaransa hivi sasa imechukua hatua mbalimbali muhimu za kuimarisha usalama katika maeneo ya nchi hiyo baada ya kushambuliwa ofisi ya gazeti la Charlie

