![]() |
| Jezi mpya ya chelsea msimu wa 2015/16 |
Siku
hiyo ya Mwaka Mpya, Straika hatari na Chipukizi wa Tottenham Harry
Kane, aliiongoza Spurs kwa kupiga Bao 2 na kutengeneza nyingine lakini
Beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, amedai safari hii washapata dawa ya
kuitandika Chelsea kwenye Fainali.
Ivanovic amedai Chelsea, ambayo itamkosa Kiungo wao Nemanja Matic aliefungiwa Mechi 2, inao uzoefu wa kucheza Fainali kupita Spurs.
Ametamba: “Tunajua nini tunapaswa kufanya. Ni Gemu ngumu lakini tupo tayari na tunaingojea kwa hamu!”
Tottenham
wametinga Fainali baada ya kuitoa Sheffield United kwa Jumla ya Mabao
3-2 kwa kushinda Mechi ya Kwanza wakiwa kwao White Hart Lane 1-0 kwa Bao
la Penati ya Andros Townsend na kisha kutoka Sare 2-2 katika Marudiano
Nyumbani kwa Sheffield United.
Nao
Chelsea walitinga Fainali baada ya kuifunga Liverpool 1-0 kwa Bao la
Dakika za Nyongeza 30 la Branislav Ivanovic wakiwa Stamford Bridge baada
ya Sare ya 1-1 katika Mechi ya Kwanza huko Anfield na kutinga Fainali
kwa Jumla ya Mabao 2-1.

