
Kamba iliotumiwa kumyonga aliyekuwa rais wa Iraq marehemu Saddam Hussein imedaiwa kuuzwa kwa zaidi ya dola millioni 4.
Kulingana na gazeti la Metro,Baadhi ya watu matajiri wanaoitaka kamba hiyo wanatoka mataifa ya Kuwait,Iran na Israel.
Kamba hiyo kwa sasa inamilikiwa na Dr Mowaffak al-Rubaie,mshauri wa usalama wa zamani nchini Iraq,ambaye aliongoza eneo ambalo rais huyo wa zamani aliuawa.
Aliamua kuihifadhi kamba hiyo baadaye na sasa anataka zaidi ya dola millioni 7 kuiuza kamba hiyo.