KAPTEIN KOMBA AFARIKI



Captain Komba enzi za uhai wake akiwa na kundi lake la TOT

  Habari zilizotufikia hivi punde , mwimbaji maarufu, mmiliki wa bendi ya Tanzania One Theatre-TOT, Mbunge wa Mbinga Magharibi na mjumbe wa Halimashauri kuu CCM Taifa, Bwana John Damiano Komba amefariki dunia ghafla kwenye Hospitali ya TMJ kwa maradhi ya Shinikizo la damu na kisukari.

Kwa Mujibu wa habari hizo na kudhibtishwa na mwanawe, bwana Komba alifariki majira ya saa 10 jioni kwa saa za Tanzania (4pm), maiti bado iko hospitali na wanafamilia wamekuwa wakizidi kumiminika  katika Hospitali hiyo.

Kaptain Komba alizaliwa Machi 18, 1954 wilayani Mbinga baada ya kusomea ualimu aliacha kufundisha na kujiunga na jeshi mwaka 1978, ambapo alipanda cheo hadi kufikia kaptaini  kabla ya kujiuzuru 1992 ili aweze kuingia kitengo cha uhamasishaji cha CCM ,

Katika kipindi chote hicho marehemu alikuwa mahiri katika kutunga nyimbo mbalimbali lakini zaidi ni zile za uhamasishaji kwa chama cha Mapinduzi
Tutaendelea kuwajuza
Displaying IMG-20150228-WA0045.jpg
Kikao cha Kamati Kuu kilisimama kwa dakika chache ili kumuombea kaptaini Komba
ONYO:Usibonyeze kuna Picha ya maiti ya marehemu kama huwezi kuangalia tafadhali usifanye hivyo.