BARCELONA YAKWEA KILELENI NA GOLI 6, SUAREZ APIGA HATRICK, MESSI ABAKIZA GOLI 1 KUMKAMATA RONALDO


Messi kafunga hat-trick leoMessi akimkacha kipa wa Rayo na kumfunga baoMessi akiwamaliza Rayo
Luis Suárez dakika ya 5 tu anaipachikia bao kwa kufanya 1-0,
Gerard Piqué kipindi cha pili aliwapachikia bao la pili na kufanya 2-0 katika dakika ya 49.

Pia Hetitriki ya Messi hii Leo imemfanya ampiku Ronaldo kwa wingi wa Hetitriki yeye sasa akiwa na 24 katika La Liga na Ronaldo ana 23.
Msimu huu wa 2014/15, Ronaldo alianza kwa moto na Mwezi Novemba alikuwa na Bao 20 za La Liga wakati Messi ana 7 tu.
Lakini tangu Mwaka 2015 uanze, Ronaldo amefunga Bao 7 tu wakati Messi amepachika Jumla ya Mabao 18 katika Mashindano yote.
Messi alipachika la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 56 kwa kufanya 3-0 dhidi ya Rayo Vallecano.
Luis Suárez aliongeza bao la nne dakika ya 63.
Lionel Messi alifunga bao lake la tatu Hat-trick dakika ya 68 na kufanya 5-0.
Luis Suarez alifunga bao lake la pili dakika za lala salama dakika ya 90 na bao la pekee la Rayo lilifungwa na A. Bueno dakika ya 81 kwa mkwaju wapenati.

VIKOSI:
Barcelona XI:
Bravo, Pique, Xavi, Pedro, Iniesta, Suarez, Messi, Mascherano, Alba, Alves, Mathieu
Akiba: Ter Stegen, Rakitic, Rafinha, Bartra, Sergi Roberto, Adriano, Munir.

Rayo XI: Álvarez, Triguero, Amaya, Ba, Insua, Trashorras, Sanchez, Ruiz, Lica, Bueno, Kakuta, Baptistao
Akiba: Cobeño, Martínez García, Contreiras Gonçalves, Aquino, Marín Ruiz, Pozuelo, Moreno Lopera