Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto’o ameweza
kutunukiwa tuzo ya kupambana na ubaguzi wa rangi juzi jumatatu na
Shirika lisilo la kiserikali la usuluhishi linalojulikana kama The European Council on Tolerance and Reconciliation (ECTR).
Ishu
ya ubaguzi wa rangi kwa nchi za wenzetu bado imeendelea kuonekana
kuchukua nafasi, hata katika soka matukio ya ubaguzi kwa baadhi ya
wanasoka ambao ni weusi imeendelea kuchukua headlines.
Tukio la hivi karibuni la mashabiki wa Chelsea lilionyesha
dhahiri kwamba wanajenga picha tofauti dhidi ya watu wa rangi nyeusi
baada ya kumzuia shabiki mwenzao asipande ndani ya treni kutokana na
kuwa mweusi.
Mchezaji huyo raia wa Cameroon
amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kupambana na mambo yanayohusu
ubaguzi kwa kipindi chote ambacho amekuwa akicheza katika klabu
mbalimbali za soka na hivi karibuni alilaani kitendo cha mashabiki wa
chelsea kumbagua shabiki mwenzao kutokana na kuwa ni mtu mweusi wakati
wakitoka uwanjani.
Eto’o ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Sampdoria ya Italy alipewa tuzo hiyo ya heshima na Shirika lisilo la kiserikali la The European Council on Tolerance and Reconciliation (ECTR)
