Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Fareed Kubanda
‘Fid Q’ ametwaa tuzo kutoka katika Umoja wa nchi za Ulaya (EU),
‘CHAMPION of the 2015 European year for Development in Tanzania’
kutokana na mchango wake katika jamii.
Akizungumzia tuzo hiyo Fid Q amesema kuwa amepewa tuzo hiyo kwa sababu maisha yake yanaonesha mfano halisi wa maisha ya wengine kwa namna ambavyo ametenga muda wake kwa ajili ya kusaidiana na jamii katika masuala ya maendeleo.
Katika hatua nyingine, Fid Q ameongeza kuwa anajiandaa kurudisha darasa la Ujamaa Hip Hop ambalo lilikuwa linafundisha vijana mbalimbali wanaojihusisha na mihadarati na wengine juu ya jinsi ya kujitoa katika janga hilo kitu ambacho ni moja ya vitu vilivyomfanya apate tuzo hiyo.