Bao 2 safi za Jordan Henderson na Phillippe Coutinho zimeendeleza
uteja wa Manchester City Uwanja wa Anfield walipochapwa Bao 2-1 na
Liverpool ambayo imepanda hadi Nafasi ya 5 na kuiacha City ikipata pigo
kubwa kutetea Ubingwa wao.
City sasa wako Pointi 5 nyuma ya Vinara Chelsea ambao wana Mechi 1 mkononi.