
Mnadhimu Mkuu Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, akitoa tamko la kumvua uanachama Zitto Zuberi Kabwe leo.
Mwanasheria mkuu wa chama cha upinzani nchini CHADEMA, Tundu Lissu leo ametangaza kuvuliwa uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kasikani Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe.
"Kwa
mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua
kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo
atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto
Kabwe sio mwanachama tena wa Chadema." Amesema Tundu Lissu
Kwa
upande wake Zitto Kabwe amesema hawakuwa na wito wa mahakamani leo na
Jaji wa kesi kahamishiwa Tabora na hawana taarifa ya Jaji Mpya, pia
kaongeza kuwa Mwanasheria anafuatilia na atatoa statement.

Waandishi wa habari wakifuatilia tukio hilo.

Lissu akitoa ufafanuzi baada ya kuulizwa maswali na wanahabari.

Katibu Mkuu wa Chadema Willbroad Slaa (kulia) akifuatilia mkutano huo wa kumvua uanachama Zitto Kabwe.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zuberi Zitto Kabwe, amevuliwa uanachama
wake mchana huu katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) jijini Dar es Salaam katika hatua iliyotangazwa na mnadhimu
mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, baada ya mbunge huyo kushindwa kesi
iliyokuwa amefungua katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi hizo, Lissu alisema
Zitto amefutwa uanachama kwa mujibu wa taratibu na sheria ya chama
isemayo kwamba endapo mwanachama atapata tatizo lolote binafsi ama la
kichama, malalamiko yote yatasuluhishwa ndani ya chama na si mahakamani
“Hivyo, kwa mujibu wa sheria za chama, Zitto alikiuka sheria anapaswa kuvuliwa uanachama wake,” alisema Lissu.
Lissu aliongeza kuwa hata kama Zitto angeweza kwenda kushitaki lazima
angeanzia katika mahakama ndogo za wilaya yaani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi au Masijala ya Mahakama ya Wilaya tofauti na alivyopeleka
kesi hiyo moja kwa moja Mahakama Kuu.
Mahakama hiyo pia imemtaka mbunge huyo wa zamani kukilipa chama hicho
gharama zote za kesi hiyo kama ilivyoelekezwa na mahakama, na kwa
mujibu wa Lissu, Chadema kitakaa na kutathmini gharama husika.
Kuhusu
utambulisho wa Zitto bungeni, Lissu alisema kwa mujibu wa kanuni za
chama chake, katibu wa chama chake anatakiwa kumwandikia barua
Mwenyekiti au Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi kumjulisha Zitto si
mwanachama wao na taratibu zingine zitafuatia.
Mpekuzi blog