Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana wa Mwaka wa PFA imekwenda kwa Straika wa Tottenham, Harry Kane mwenye Miaka 21.
Msimu huu, Hazard, mwenye Miaka 24, amefunga Mabao 13 kwa Chelsea
na kutengeneza Bao 8 katika Mechi 33 za Ligi Kuu England na kuisaidia
Timu yake kuukaribia Ubingwa.
Mshindi wa Tuzo za PFA huchaguliwa kwa Kura za Wachezaji wenzake wa Kulipwa.
Hazard, ambae Msimu uliopita ndie alikuwa Mshindi wa Tuzo ya
Mchezaji Bora Kijana wa PFA, alikabidhiwa Tuzo yake Jana huko Grosvenor
Hotel Jijini London.
Awali Jana, Hazard alichaguliwa mmoja wa Wachezaji 6 wa Chelsea kwenye Kikosi cha PFA, cha Timu Bora ya Mwaka.
Wachezaji wengine wa Chelsea kwenye Kikosi hicho ni Mabeki
Branislav Ivanovic, John Terry na Gary Cahill na Viungo Nemanja Matic
pamoja na Straika Diego Costa.
Wachezaji wengine waliounda Kikosi hicho cha Wachezaji 11 ni
Fulbeki wa Southampton Ryan Bertrand, Straika wa Tottenham Harry Kane,
Philippe Coutinho wa Liverpool, Alexis Sanchez wa Arsenal na Golikipa wa
Manchester United David De Gea.
LISTI KAMILI YA WAGOMBEA:
-MCHEZAJI BORA WA MWAKA
Diego Costa (Chelsea)
David De Gea (Manchester United)
Philippe Coutinho (Liverpool)
Eden Hazard (Chelsea)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)
Alexis Sanchez (Arsenal)
-MCHEZAJI BORA KIJANA WA MWAKA
Thibaut Courtois (Chelsea)
Philippe Coutinho (Liverpool)
David De Gea (Manchester United)
Eden Hazard (Chelsea)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)
Raheem Sterling (Liverpool)