CARLO ANCELOTTI AFUKUZWA RASMI REAL MADRID

1388001821_extras_mosaico_noticia_1_g_0
RASMI: Real Madrid imevunja mkataba na kocha wake Carlo Ancelotti baada ya kuinoa kwa miaka miwili.
 
Katika msimu wake wa kwanza Bernabeu, Ancelotti alishinda ligi ya mabingwa, Copa del Rey,  Uefa Super Cup na kombe la klabu bingwa  ya FIFA duniani.
Ancelotti ameshindwa kushinda medali msimu huu na kumaliza pointi mbili nyuma ya mabingwa FC Barcelona.
 
Kocha wa Napoli, Rafael Benitez anapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Ancelotti.
 
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amethibitisha kufukuzwa kwa Carlo na anatarajia kutangaza mrithi wake juma lijalo.