Picha,Barcelona na mashabiki wake walivyomuaga Xavi.
Wachezaji wa timu ya Barcelona wamevalia jezi maalum katika mechi yao ya mwisho ya msimu huu ili kutoa heshima kwa kiungo wao wa kati Xavi ambaye anakamilisha uhusiano wake wa miaka 24 na klabu hiyo .
Xavi amepewa kwaheri maalum katika mechi dhidi ya Deportivo la Coruna iliyochezwa katika uwanja wa Nou Camp siku ya jumamosi.
Xavi mwenye umri wa miaka 35 ambaye amejishindia medali yake ya nane ya la liga alitangaza siku ya alhamisi kwamba ataondoka Barcelona mwishoni mwa msimu huu ili kujiunga na kilabu ya Qatar Al Saad. Xavi alisema uamuzi huo umekuwa mgumu kwake.