
Messi akishangilia goli la ubingwa
LIONEL Messi amewapa Barcelona
ubingwa wa La Liga msimu wa 2014/2015 baada ya kuifungia bao pekee
katika ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Atletico Madrid kwenye uwanja wa
Vicent Calderon.
Messi amefunga goli hilo katika dakika ya 65′ akimalizia pasi ya Pedro Rodriguez.
Kwa matokeo hayo Barcelona wamefikisha pointi 93 baada ya kushuka dimbani mara 37 na wamebakiza mechi moja.
Real Madrid wameshinda magoli 4-1 dhidi ya Espanyol na kufikisha pointi 89 katika mechi 37 walizocheza.
Kwa maana hiyo wakishinda mechi ya mwisho watafikisha pointi 92 ambazo tayari zimeshavukwa na Barcelona .
Inawezekana msimu ukawa mkubwa
kwa Barcelona, leo wameshatwaa taji la ligi kuu, La Liga na watacheza
fainali mbili, ligi ya mabingwa ulaya na kombe la mfalme ‘Copa del Rey’.
Licha ya kuugulia maumivu ya
kutolewa nusu fainali ya Uefa na Juvuntes katikati ya wiki hii na leo
kukosa ubingwa wa La Liga, mshambuliaji hatari wa Real Madrid, Cristiano
Ronaldo amefunga magoli matatu peke yake ‘hat-trick’ katika ushindi wa
Madrid.
Ronaldo amefunga magoli hayo
katika dakika ya 59′, 83′ na 90′. Goli lingine limefungwa na Marcelo
dakika ya 79′ wakati goli la kufutia machozi kwa Espanyol limefungwa na
Cristian Stuani dakika ya 73”.
