
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Barani Afrika -CAF leo hii limeipa Tanzania uenyeji wa fainali za
michuano ya Afrika ya vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.
Uenyeji huu ni hatua muhimu sana
kwa Tanzania katika kukuza soka la vijana na kwa hatua hii Tanzania
itacheza moja kwa moja fainali hizi.
Katika kuandaa kikosi bora cha
kushiriki fainali hizi Tanzania, mwezi Juni mwaka huu TFF itaandaa
mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 na wachezaji bora
wa mashindano haya wataunda kikosi cha mwanzo cha Taifa kuelekea fainali
za mwaka 2019.
TFF inamshukuru sana Rais Jakaya
Kikwete na Mh. Fennela Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo kwa kufanikisha maamuzi haya, na inaamini ushirikiano huu wa
Serikali na wadau wengine utafanikisha mashindano haya mwaka 2019.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)