Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Kikwete ameshasaini miswada 9 katika ya 14 iliyopitishwa na bunge katika mkutano wake wa 19 ukiwemo wa sheria ya makosa ya mitandao pamoja na muswada wa sheria ya takwimu iliyozua utata.
Akitoa taarifa kuhusu kusainiwa kwa miswada hiyo leo Bungeni Spika wa
Bunge Anna Makinda amesema miswada mitano iliyobaki atatolea ufafanuzi
baada ya kupata kibali kutoka kwa Rais.
Makinda ametaja Miswada mingine iliyosainiwa ni pamoja na Muswada wa
Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, Muswada wa Sheria ya Tume ya
Kudhibiti UKIMWI, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya
Stakabadhi Ghalani, Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Silaha, Muswada wa
Sheria ya Miamala ya Kiektoniki pamoja na Muswada wa Sheria ya Baraza la
Vijana la Taifa.
Mpekuzi blog