
Mmiliki huyu wa Taylor Gang ametumia twitter kusema kuwa album itaitwa Rolling Papers 2: The Weed Album,ambayo ni muendelezo wa album yake ya mwaka 2011 Rolling Papers, iliyokuwa na wimbo kama “Black and Yellow.”
Rolling Papers 2 inakuja baada ya album ya mwaka 2014 Blacc Hollywood, iliyoshika namba moja kwa kuuza kopi 90,000 ndani ya wiki ya kwanza