
MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi amesema kuwa taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye amejitoa kwa Lowasa si za kweli.
Alisema hayo kwa waandishi wa habari, aliokutana nao jijini Dar es Salaam, jana.
Alikutana
na waandishi hao ili kufafanua kuhusu taarifa, aliyosema inaenezwa
kupitia mitandao ya kijamii, yenye kichwa cha habari ‘Mengi ajitoa rasmi
kwa Lowassa’. Edward Lowassa ni mgombea urais wa Chadema anayeungwa
mkono na vyama vinavyounda Ukawa.
Mbali na Chadema, vyama vingine katika Ukawa ni CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.
Taarifa yake aliyosoma kwa waandishi wa habari kuhusu suala hilo ilisema: “Nimeomba
tukutane leo kwa jambo moja tu. Kuwafahamisha kwamba taarifa
inayoenezwa kupitia mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari
kinachosema ‘Mengi ajitoa rasmi kwa Lowassa’ na eti nimesema ‘kama hawa
jamaa (Ukawa) watashinda nafasi ya Urais, basi ni baada ya miaka 10 siyo
hivi sasa,” alisema.
Dk Mengi alisema
“Taarifa hiyo ni ya uongo, upotoshaji na uchochezi”. Dk Mengi alieleza
kuwa “Taarifa za aina hii zisipokemewa na kuchukuliwa hatua za haraka,
zitaathiri amani ya Taifa letu. Ni matarajio yangu kwamba vyombo husika
vitachukua hatua zinazostahili kwa haraka iwezekanavyo”.

Mpekuzi blog
