![]() |
Mbwana Samatta leo amesaidia Tanzania kuitoa Malawi mbio za Kombe la Dunia 2018 Urusi |
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta kwa mara ya pili ameingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Anayecheza Afrika.
Taarifa
ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
imetoa orodha zote mbili za Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika na Mwanasoka
Bora wa Mwaka Anayecheza Afrika.
Katika
tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Anayecheza Afrika, Samaatta mwenye umri
wa miaka 23 anachezea TP Mazembe ya DRC, anachuana na Abdeladim
Khadrouf wa Moghreb Tetouan ya nyumbai, Morocco, Abdelmalek Ziaya wa ES
SETIF ya nyumbani, Algeria, Ahmed Akaichi wa Esperance ya nyumbani,
Tunisa, Andiramahitsinoro Carolus wa Madagascar anayechezea USMA ya
Algeria na Baghdad Bounedjah wa Algeria anayechezea Etoile du Sahel ya
Tunisia.
Wengine
ni Bakri el Madina wa El Merriekh ya nyumbani, Sudan, Bassem Morsi wa
Zamalek ya nyumbani, Misri, Boris Moubhio wa AC. Leopards ya nyumbani,
Kongo-Brazzaville, Djigui Diarra wa Stade Malien ya nyumbani, Mali na
Felipe Ovono wa Guinea anayechezea Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Wamo pia Guelassiognon Sylvain
Gbohouo
wa Ivory Coast anayecheza na Samatta T.P Mazembe, Hazem Emam wa Zamalek
ya nyumbani, Misri, Hocine Ragued wa Esperance ya nyumnbani, Tunisia,
Kermit Erasmus wa Orlando Pirates ya nyumbani Afrika Kusini na Malick
Evouna wa Gabon, anayechezea Al Ahly ya Misri.
Wamo
pia Mohamed Koffi wa Burkina Faso anayechezea Zamalek ya Misri, Mohamed
Meftah wa USMA ya nyumbani, Algeria, Moudather el Tahir wa El Hilal ya
nyumbani, Sudan, Oupa Manyisa wa Orlando Pirates ya nyumbani Afrika
Kusini, Robert Kidiaba wa T.P Mazembe ya nyumbani, DRC, Roger Assale wa
Ivory Coast anayechezea T.P Mazembe, Thamsanqa Gabuza wa Orlando Pirates
ya nyumbani Afrika Kusini na
Zein Edin Farahat wa USMA ya nyumbani, Algeria.
Katika
tuzo Ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika, Yaya Toure wa Ivory Coast na
Manchester City ataitetea dhidi ya Ahmed Musa wa CSKA Moscow ya Urusi na
Nigeria, Andre Ayew wa Swansea City ya England na Ghana, Aymen
Abdennour wa FC Valence ya Hispania na Tunisia, Baghdad Bonjah wa Etoile
du Sahel ya Tunisia na Algeria.
Wengine
ni Bassem Morsi wa Zamalek ya Misri, Chrisitian Atsu wa Bournemouth ya
England na Ghana, Dieu Merci Mbokani wa Norwich ya England na DRC, El
Arbi Hillel Soudani wa Dynamo Zagreb ya Croatia na Algeria, Faouzi
Ghoulam wa Napoli ya Italia na Algeria na Ferebory Dore wa Angers ya
Ufaransa na Kongo.
Wamo
pia Gervais Yao Kouassi wa Rome ya Italia na Ivory Coast, Ibrahima
Traore wa Borussia Monchengladbach ya Ujerumani na Guinea, Javier Balboa
wa Al-Faisaly ya Saudi Arabia na Equatorial Guinea, Heldon Ramos wa Rio
Ave ya Ureno na Cape Verde, Mame Diouf wa Stoke City ya England na
Senegal.
![]() |
Yaya Toure ateteta tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa Afrika |
Wamo
pia Max Alain Gradel wa Bournemouth ya England na Ivory Coast, Mehdi
Benatia wa Bayern Munich ya Ujerumani na Morocco, Modather Al Tayeb
“Karika” wa El Hilal ya Sudan, Mohamed Salah wa AS Roma ya Italia na
Misri, Nicolas Nkoulou wa Marseille ya Ufaransa na Cameroon na
Pierre-Emerick Aubameyang wa Borussia Dortmund ya Ujerumani na Gabon.
Wengine ni Robert Kidiaba wa T.P Mazembe,
Rudy
Gestede wa Aston Villa ya England na Benin, Riyad Mahrez wa Leicester
City ya England na Algeria, Sadio Mane wa Southampton ya England na
Senegal, Serge Aurier wa Paris Saint Germain ya Ufaransa na Ivory Coast
na Seydou Keita wa Rome ya Italia na Mali.
Wengine
ni Sofiane Feghouli wa Valencia ya Hispania na Algeria, Stephane Mbia
wa Trabzonspor ya Uturuki na Cameroon, Thievy Bifouma wa Granada ya
Hispania na Kongo, Victor Wanyama wa Southampton ya England na Kenya na
Vincent Aboubakar wa Porto ya Ureno na Cameroon.
Wengine
ni Vincent Enyeama wa Lille ya Ufaransa na Nigeria, Yacine Brahimi wa
Porto ya Ureno na Algeria, Yannick Bolasie wa Crystal Palace ya England
na DRC na Yasine Chikhaoui wa Al-Gharafa ya Qatar na Tunisia.