
Leo
Rais John Magufuli ameongoza Watanzania kutumia Siku ya Uhuru kufanya
usafi, yuko eneo la ufukwe karibia na Ikulu akifanya usafi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa naye yuko kwenye soko la Kariakoo akiongoza wafanyabiashara wa soko hilo kufanya usafi.
Ni
siku ya kihistoria kwa taifa tofauti na ilivyokuwa imezoeleka kwamba
siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania watu huelekea viwanja vya Uhuru
kuungana na wengine kuadhimisha siku hii ambapo leo ni miaka 54 tangu
uhuru kupatikana,lakini watu wanafanya usafi kuboresha mazingira
ikielezwa ni UHURU na KAZI,ikienda sambamba na kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu

Mpekuzi blog