CHELSEA &ARSENAL WAFUZU CHAMPIONS LIGUE.... Tazama video za magoloi yao hapa

wamevuka 1
Chelsea imefuta machungu ya vipigo vya ligi ya ndani (EPL) baada ya kufanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya hatua ya mtoano baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya FC Porto.

The Blues wamefurahia ushindi wa nyumbani kwa kuitupa nje ya mashindano Porto, bao la kujifunga la Ivan Marcano liliipa Chelsea nafasi ya kuongoza. Porto ilikuwa ikihitaji ushindi pekee ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo lakini ilishindwa kupata ushindi kwenye mchezo huo mbele ya CVhelsea ambayo haiku kwenye wakati mzuri tangu kuanza kwa ligi ya England msimu huu.

Willian aliihakikishia Chelsea nafasi ya kuongoza kundi G baada kufunga goli la pili akiwa umbali wa zaidi ya mita 20 kutoka langoni mwa Porto.


ARSENAL YASHINDA 3 BILA
wamevuka
Masiharamasihara hatimaye Arsenal imefanikiwa kutinga hatua ya mtoano (16 bora) kufuatia hat-trick ya Olivier Giroud wakati Arsenal ikicheza ugenini dhidi ya Olympiacos na kuwafungisha virago wagiriki hao kwenye michuano ya UEFA Champions League.

Giroud alianza kuing’arisha Arsenal kwa goli lake la kichwa dakika ya 29 akiunganisha mpira uliopigwa na Aron Ramsey goli lililodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili Giroud aliendeleza kuwafurahisha wapenzi wa The Gunners baada ya kufunga goli la pili dakika ya 49 akipokea pasi safi toka kwa Campbell lakini Giroud akalizamisha jahazi la Olympicos kwa kupiga goli la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Olympiacos kuunawa mpira akiwa kwenye eneo la hatari.

Hiyo ni hat-trick ya kwanza kwa Giroud tangu ajiunge na miamba ya London lakini hat-trick hiyo ndiyo imeipeleka Arsenal kwenye hatua ya mtoano.

Arsena imeendeleza rekodi yake ya kufuzu kwa hatua ya mtoano, The Gunners haijawahi kushindwa kufuzu kutoka hatua ya makundi kwenda hatua ya mtoano tangu msimu wa 2003-04.

Angalia magoli yote aliyofunga Olivier Giroud kupitia Dauda TV na kuifanya Arsenal kufuzu kwa hatua ya mtoano.