Mgombea urais wa chama cha
Republican nchini Marekani, Donald Trump, amezua mjadala mpya baada ya
kuwahimiza wafuasi wake wenye bunduki kumzuia mgombea wa chama cha
Democratic Hillary Clinton, kubatilisha haki yao ya kikatiba ya kumiliki
silaha.
Bw Trump alikuwa akihutubu katika mkutano wa siasa katika jimbo la North Carolina.
Bw
Trump alikuwa amesema kwamba iwapo Bi Clinton atashinda basi atateua
majaji wa Mahakama ya Juu ambao watafanikisha kuondolewa kwa haki ya
raia kumiliki bunduki.
Alidokeza kwamba ni hatua ya raia pekee, ambayo inaweza kuzuia hilo lisifanyike.
Maafisa wa kampeni wa Clinton wameshutumu matamshi ya Trump na kusema ni hatari.