Chama cha Republican cha Rais wa Marekani, Donald Trump kimeibuka washindi wa uchaguzi wa bunge la Congress.
Uchaguzi wa jimbo la Georgia ndio umeteka vichwa vingi kutokana na
kugharimu fedha nyingi katika kampeni zake ambapo Bi. Karen Handel,
ambaye ni mgombea wa Republican ameshinda kwa asilimia 53 ya kurra
zilizopigwa huku mgombea wa Democratic akijipati asilimia 47 ya kura
hizo.
Spika wa bunge la Marekani Paul Ryan alimpongeza Bi Handel kwa
ushindi huo mnono ambapo mwanzoni chama cha Democratic kilitegemea
kushinda kwenye uchaguzi huo kutokana na kushuka kwa umaarufu wa Trump
kwenye jimbo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotoka inadai, jumla ya dola milioni 56
zinakadiriwa kutumika katika uchaguzi huo katika jimbo la Georgia na
ndio inasemekana ndio uchaguzi uliogharamikiwa katika historia ya
Marekani.

