UNAI EMERY ATEULIWA RASMI KUMRITHI WENGER ARSENAL


Ni rasmi sasa uongozi wa klabu ya Arsenal umemtangaza Kocha Unai Emery kurithi mikoba ya Arsene Wenger aliyekaa na kikosi kwa muda mrefu.

Emery amekabidhiwa kiti cha Wenger ambaye alitangaza kustaafu baada ya kuitumikia kwa zaidi ya miaka 20 

Emery anawasili Arsenal akitokea PSG ya Ufaransa aliyoifikisha hatua ya makundi na kutolewa kwenye ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu.

Kocha huyo ataanza rasmi majukumu ya kukiandaa kikosi cha Arsenal kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.