Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, amewataka wafuasi wake wasihuzunike na hatua ya yeye kuwekwa rumande kwa madai ya kutopatiwa dhamana bali watumie nafasi hiyo kuombea tume huru ya uchaguzi.
Kauli
 hiyo ya Mbowe imetolewa Jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa 
chama hicho bara na mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika wakati 
akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya kusikilizwa rufaa ya
 kupata au kutopata dhamana kwa viongozi hao wawili.
"Mwenyekiti
 amesisitiza sana, kutomlilia yeye bali walilie taifa letu kutafuta 
mabadiliko, kudai tume huru ya uchaguzi, kwa sababu kesi hii msingi wake
 ni uchaguzi uliosababisha kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Akwilina kwa hiyo
 naomba wajitokeze kwa waingi kesho," amesema Mnyika.
Wakati
 huohuo Mnyika amebainisha kuwa chama hicho kupitia mawakili wake 
kimewasilisha maombi ya kuiomba mahakama kutoa kipaumbele kwa kesi dhdi 
ya viongozi wake kabla ya mahakama hiyo haijaenda likizo.

