Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) la
mfutia usajili msanii wa muziki wa Bongo Fleva Godfrey Tumaini maarufu
kama Dudu Baya kuanzia jana April 16, 2020.
Hatua imetokana na kitendo cha msanii
huyo kutumia lugha za matusi kwa wadau wa sanaa kupitia akaunti yake ya
Instagram huku akitambua fika kuwa yeye ni msanii aliyesajiliwa na
BASATA.