Katika hali isiyo ya kawaida mzee mwenye
umri wa miaka 80 ameomba msaada wa serikali kuingilia kati na kuzuia
mtoto wake kuuza shamba lake ambalo alilichimba zaidi ya miaka 35
iliyopita.
Shamba lenyewe lipo Mathira Kenya ambapo mzee analalamika kwamba
mtoto wake wa kiume amekuwa akiuza sehemu ya shamba hilo kidogo kidogo.
Amesema tofauti na matarajio yake alikuwa akiamini Mtoto huyo
angekuja kumsaidia uzeeni lakini ndio amekuwa akiuza shamba hilo bila
ruhusa yake na kuhofia kuwa anaweza kuuza hata kipande cha shamba
ambacho amechijimbia kaburi lake.