Waziri Mwakyembe aliyasema hayo bungeni wakati akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya wizara yake.
"Tembea dunia kote huko, nimekwenda Nigeria na kuona wasanii wakubwa kama Tiwa Savage, Don Jazz, Akon, P Square wale hawaimbi kuhusu viongozi wao wa kisiasa.
"Hivyo niwasihi wasanii wangu, muache kuimba kuhusu siasa sababu hii ni ‘entertainment industry’ (sekta ya burudani) na sio ya masuala ya kisiasa, "alisema Waziri Mwakyembe.
Aidha, waziri alisema kama kuna msanii yeyote anayetaka kuwa mwanasiasa aache muziki akagombee udiwani kwani wasanii waliotaka kuchanganya siasa na muziki walipotea kabisa.